Orodha ya Madiwani
Madiwani ni wawakilishi wa wananchi waliochaguliwa katika majimbo mbalimbali ya Wilaya ya Kati. Wanafanya kazi ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Muundo wa Baraza la Madiwani
Kwa mujibu wa Sheria Na. 17 ya mwaka 2014, Baraza la Manispaa Kati lina aina tatu za madiwani:
Madiwani wa Kuchaguliwa
Madiwani wanaochaguliwa na wananchi kutoka katika wadi 8 za Wilaya ya Kati:
Madiwani Wateule
Madiwani 5 wanaoteuliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi Maalum vya SMZ.
Viti Maalum vya Wanawake
Madiwani watatu (3) wa viti maalum vya wanawake.
Mhe. Said Hassan Shaaban
Jimbo la Wadi ya Koani
Mhe. Said Hassan Shaaban ni Diwani wa Wadi ya Koani katika Wilaya ya Kati, Unguja. Pia anahudumu kama Meya wa Baraza la Manispaa Kati. Katika nafsi yake ya uongozi, anawajibika kuwakilisha wananchi wa Wadi ya Koani, kushauri na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kushiriki maamuzi yanayohusu maendeleo ya Manispaa na Wilaya ya Kati.
Mhe. Haji Mzee Ali
Jimbo la Wadi ya Kiboje
Mhe. Haji Mzee Ali ni Diwani wa Wadi ya Kiboje. Ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa Wadi ya Kiboje kuwakilisha maslahi yao katika Baraza la Manispaa Kati na kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika wadi hiyo.
Mhe. Abdulrahman Ali Abdalla
Jimbo la Wadi ya Bambi
Mhe. Abdulrahman Ali Abdalla, Diwani wa Wadi ya Bambi, ni mwakilishi wa wakazi wa Bambi aliyechaguliwa kusimamia na kulinda maslahi ya wakazi wa wadi hiyo katika Baraza la Manispaa Kati. Anawajibika kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuhimiza ushiriki wa wananchi wa Bambi katika shughuli za kijamii na kiuchumi, pamoja na kushughulikia changamoto zinazowakabili wakazi wa wadi hiyo.
Mhe. Seif Hamad Seif
Jimbo la Wadi ya Bungi
Mhe. Seif Hamad Seif ni Diwani aliyechaguliwa na wananchi wa Wadi ya Bungi. Anashiriki kikamilifu katika vikao vya Baraza la Madiwani na anachangia mipango ya maendeleo, ushauri na usimamizi wa shughuli za Manispaa kwa manufaa ya wananchi wa wadi yake.
Mhe. Hamida Bahati Giri
Jimbo la Wadi ya Cheju
Mhe. Hamida Bahati Giri ni Diwani wa Wadi ya Cheju. Anajitahidi kuwakilisha maslahi ya wananchi wa Wadi ya Cheju katika Baraza la Manispaa Kati na kushiriki katika kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo.
Mhe. Ali Hassan Mambo
Jimbo la Wadi ya Chwaka
Mhe. Ali Hassan Mambo ni Diwani wa Wadi ya Chwaka. Anawakilisha maslahi ya wananchi wa Wadi ya Chwaka na kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya Baraza la Manispaa Kati yanayohusu maendeleo ya wilaya.
Mhe. Hadhar Abdalla Hadhar
Jimbo la Wadi ya Tunguu
Mhe. Hadhar Abdalla Hadhar ni Diwani wa Wadi ya Tunguu na pia anahudumu kama Naibu Meya wa Baraza la Manispaa Kati. Anashiriki katika uongozi wa Baraza na kusimamia maendeleo ya Wadi ya Tunguu na Wilaya ya Kati kwa ujumla.
Mhe. Ussi Mtumwa Ali
Jimbo la Wadi ya Ubago
Mhe. Ussi Mtumwa Ali ni Diwani wa Wadi ya Ubago. Anawakilisha wananchi wa Wadi ya Ubago na kushiriki katika mipango na maamuzi ya Baraza la Manispaa Kati.
Mhe. Hidaya Said Hamad
Jimbo la Kiti Maalum
Diwani wa Kiti Maalum anashiriki kikamilifu katika vikao vya Baraza la Madiwani na anachangia mipango, ushauri na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Mhe. Tendani Mkanga Miraji
Jimbo la Kiti Maalum
Diwani wa Kiti Maalum anashiriki kikamilifu katika vikao vya Baraza la Madiwani na anachangia mipango, ushauri na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Mhe. Riziki Abdalla Mohamed
Jimbo la Kiti Maalum
Diwani wa Kiti Maalum anashiriki kikamilifu katika vikao vya Baraza la Madiwani na anachangia mipango, ushauri na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Mhe. Said Mtaji Askari
Jimbo la Uteuzi wa Waziri
Diwani wa Uteuzi wa Waziri ni mwanachama wa Baraza la Madiwani aliyeteuliwa na Waziri anayehusika na Serikali za Mitaa kwa mujibu wa sheria husika. Uteuzi huu unafanywa kwa lengo la kuimarisha uwakilishi, kuongeza utaalamu katika masuala ya maendeleo, na kuchangia uongozi na usimamizi wa shughuli za baraza au manispaa.
Mhe. Catherine Peter Nao

Mhe. Amina Adrew Clement

Mhe. Ghania Ali Makame

Mhe. Juma Kumba