Baraza
Baraza la Manispaa Kati
Zanzibar
SMZ
Baraza la Manispaa Kati
+255 773 168 121
|
Nyingine 2026/2027

Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027

Bajeti ya Manispaa Kati kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imeandaliwa kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, kuboresha miundombinu, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani, na kutekeleza miradi ya maendeleo inayowafaidisha wananchi. Bajeti hii inaakisi vipaumbele vya maendeleo ya Manispaa kulingana na mahitaji ya jamii na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mkakati 2025/2026

Kampeni ya Safisha, Pendezesha Wilaya ya Kati

Kampeni ya "Safisha na Pendezesha Wilaya ya Kati" ni programu ya kuhamasisha wananchi, taasisi za umma na binafsi, vikundi vya jamii, na wadau mbalimbali kushiriki katika usafi wa mazingira na uboreshaji wa mandhari katika Wilaya ya Kati. Kampeni hii inalenga kuunda mazingira safi, salama, yenye afya na yenye kuvutia kwa wakazi na wageni.