Machapisho Rasmi
Nyingine
2026/2027
Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027
Bajeti ya Manispaa Kati kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imeandaliwa kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, kuboresha miundombinu, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani, na kutekeleza miradi ya maendeleo inayowafaidisha wananchi. Bajeti hii inaakisi vipaumbele vya maendeleo ya Manispaa kulingana na mahitaji ya jamii na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.