Fursa za Uwekezaji
Wilaya ya Kati inatoa mazingira bora ya uwekezaji. Wasiliana nasi kwa habari zaidi kuhusu fursa zinazopatikana.
Uwekezaji wa Biashara — Tunguu na Jumbi
Shehia ya Tunguu ina mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara katika sekta za huduma, kilimo, usafiri, ujenzi, na teknolojia. Kwa kutumia fursa hizi, wananchi wanaweza kuongeza mapato yao, kuunda ajira, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Wilaya ya Kati.
Uwekezaji wa Biashara na Utalii — Jumbi
Shehia ya Jumbi ni mojawapo ya maeneo yenye ukuaji mkubwa wa makazi na uchumi katika Wilaya ya Kati. Kutokana na ukaribu wake na Mji wa Zanzibar na miundombinu ya barabara, Shehia ya Jumbi ina mazingira mazuri ya kuendeleza kilimo, ufugaji, huduma, na biashara ndogo na za kati. Pia ina fursa mbalimbali za utalii kutokana na urithi wake wa kiutamaduni, mazingira ya asili, shughuli za kilimo, na ukaribu wake na maeneo muhimu ya Zanzibar.
Bustani ya Hanyegwa
Ofisi ya Baraza la Mji Kati imeweza kupiga hatua kwa kuweka sehemu ya kitalu (bustani) ambayo ni sehemu moja wapo ya chanzo cha mapato na kivutio kwa wageni wanaokuja kupata huduma katika Ofisi hiyo. Baraza la Mji Kati linatoa huduma za bustani za aina zote kama vile miche ya aina ya michungwa, midimu, mifenesi na miparachichi.
Bustani ya Kwa Bihole
Ofisi ya Baraza la Mji Kati imeweza kupiga hatua kwa kuweka sehemu ya kitalu (bustani) ambayo ni sehemu moja wapo ya chanzo cha mapato na kivutio kwa wageni wanaokuja kupata huduma katika Ofisi hiyo. Baraza la Mji Kati linatoa huduma za bustani za aina zote kama vile miche ya aina ya michungwa, midimu, mifenesi na miparachichi. Kumbukumbu: Bustani ya Kwa Bihole kwa sasa siyo mali ya Baraza la Mji Kati.
Fursa za Utalii katika Wilaya ya Kati
Wilaya ya Kati ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo alama za kihistoria, magofu, mapango na maeneo ya asili yenye uzuri wa pekee. Baraza la Mji Kati linakusudia kuendeleza sekta ya utalii ili kuleta faida kwa wananchi na kuongeza pato la Wilaya.
Soko la Dunga
Kupitia makusanyo ya ndani ya Baraza la Mji Kati limeweza kuwekezea sehemu za kibiashara katika kukuza pato la taasisi na Serikali kiujumla kwa kujenga masoko na maduka mbalimbali katika Wilaya ya Kati.
Soko la Kikungwi

Maduka ya Kipilipilini (Maduka ya Chwaka)
Kupitia makusanyo ya ndani ya Baraza la Mji Kati limeweza kuwekezea sehemu za kibiashara katika kukuza pato la taasisi na Serikali kiujumla kwa kujenga masoko na maduka mbalimbali katika Wilaya ya Kati.
Maduka ya Temeke Dunga