Fursa za Uwekezaji
Wilaya ya Kati inatoa mazingira bora ya uwekezaji. Wasiliana nasi kwa habari zaidi kuhusu fursa zinazopatikana.
Uwekezaji wa Biashara na Utalii — Jumbi
Shehia ya Jumbi ni mojawapo ya maeneo yenye ukuaji mkubwa wa makazi na uchumi katika Wilaya ya Kati. Kutokana na ukaribu wake na Mji wa Zanzibar na miundombinu ya barabara, Shehia ya Jumbi ina mazingira mazuri ya kuendeleza kilimo, ufugaji, huduma, na biashara ndogo na za kati. Pia ina fursa mbalimbali za utalii kutokana na urithi wake wa kiutamaduni, mazingira ya asili, shughuli za kilimo, na ukaribu wake na maeneo muhimu ya Zanzibar.
Fursa za Utalii katika Wilaya ya Kati
Wilaya ya Kati ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo alama za kihistoria, magofu, mapango na maeneo ya asili yenye uzuri wa pekee. Baraza la Mji Kati linakusudia kuendeleza sekta ya utalii ili kuleta faida kwa wananchi na kuongeza pato la Wilaya.